WAZIRI MKUU ASHIRIKI CHAKULA NA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM, ASISITIZA UPENDO NA WAJIBU WA JAMII

WAZIRI MKUU ASHIRIKI CHAKULA NA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM, ASISITIZA UPENDO NA WAJIBU WA JAMII
▪︎ Asema hakuna mtoto anayepaswa kuachwa nyuma ▪︎ Aelekeza vituo vyote vitambuliwe na kuimarishwa Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema hakuna mtoto anayepaswa kuachwa nyuma katika jamii, akisisitiza kuwa kuwahudumia watoto wenye mahitaji maalum si hisani bali ni wajibu wa pamoja wa jamii na Taifa kwa ujumla. Ameyasema hayo Aprili 6, 2026, alipojumuika na watoto wenye mahitaji maalum katika chakula cha pamoja kilichoandaliwa katika makazi yake ya Oysterbay jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Pasaka.  “Kufanya tukio la aina hii si hisani bali ni wajibu kama ambavyo hata maandiko matakatifu yanatutaka kufanya hivyo kuwahudumia wenye uhitaji,” amesema. Amesema Pasaka ni fursa ya kuenzi na kuendeleza matendo ya upendo, huruma na mshikamano kwa vitendo, huku akiwahimiza Watanzania kuendeleza maadili hayo katika maisha ya kila siku. “Leo tunapata fursa ya kutafakari kwa kina juu ya wajibu wetu wa kuendeleza matendo ya huruma, upendo na mshikamano katika jamii yetu,” amese…