WAZIRI MKUU AKAGUA MADHARA YA MOTO SOKO LA SIMU 2000, AAGIZA HATUA ZA HARAKA KUREJESHA BIASHARA

WAZIRI MKUU AKAGUA MADHARA YA MOTO SOKO LA SIMU 2000, AAGIZA HATUA ZA HARAKA KUREJESHA BIASHARA
-Asema Serikali itatoa kauli baada ya uchunguzi -Aagiza vibanda vipya vigawiwe kwa wafanyabiashara halisi WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameagiza hatua za haraka kurejesha shughuli za biashara kufuatia ajali ya moto ulioteketeza Soko la Mawasiliano (Simu 2000) lililopo katika Kata ya Sinza, Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam. Ameyasema hayo Aprili 6, 2026, alipofika kukagua madhara ya tukio hilo la moto lililotokea Aprili 4, 2026, ambapo takribani vibanda 500 vya wafanyabiashara wadogo viliteketea. Akizungumza na wafanyabiashara hao, Waziri Mkuu amesema Serikali inaendelea kufuatilia kwa karibu tukio hilo na itatoa kauli rasmi baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa kina ulioelekezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. “Mheshimiwa Rais amepata taarifa ya jambo hili, anawapa pole sana na ameelekeza uchunguzi wa kina ufanyike ili tujue chanzo cha tatizo hili. Na kazi hiyo imekwisha kuanza ili tuweze kupata undani wa chanzo cha jambo hili lili…