Waziri Kombo Ashiriki Mkutano wa Tisa wa Bahari ya Hindi Mauritius
Waziri Kombo Ashiriki Mkutano wa Tisa wa Bahari ya Hindi Mauritius
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mahmoud Thabit Kombo ameshiriki Mkutano wa Tisa wa Bahari ya Hindi, unaofanyika jijini Port Louis, Mauritius Aprili 10 hadi 12, 2026. Mkutano huo unawakutanisha viongozi wa serikali, wanadiplomasia, wataalamu wa masuala ya usalama wa bahari, pamoja na wadau wa maendeleo kutoka mataifa yanayozunguka Bahari ya Hindi kujadili fursa na changamoto zinazohusiana na usalama wa bahari, biashara, mabadiliko ya tabianchi, pamoja na ushirikiano wa kiuchumi katika ukanda wa Bahari ya Hindi. Mkutano huo umefunguliwa na Waziri Mkuu wa Mauritius Mheshimiwa Dr. Navinchandra Ramgoolam aliyesisitiza umoja, ushirikiano, na uwajibikaji wa pamoja miongoni mwa mataifa ya Bahari ya Hindi. Ametoa wito kwa nchi kushirikiana kukabiliana na changamoto za pamoja kama vile vitisho vya usalama, mabadiliko ya tabianchi, na maendeleo ya kiuchumi, ili kujenga mustakabali salama, endelevu, na wenye ustawi kwa eneo hilo. Akizungumza katika ufunguzi wa Mkuta…