WAZIRI KOMBO AKUTANA NA RAIS WA RWANDA, PAUL KAGAME

WAZIRI KOMBO AKUTANA NA RAIS WA RWANDA, PAUL KAGAME
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame, katika Kijiji cha Urugwiro tarehe 1 Aprili, 2026. Katika mazungumzo hayo, viongozi hao wamejadili namna ya kuimarisha uhusiano imara uliopo kati ya Tanzania na Rwanda, huku wakisisitiza umuhimu wa kukuza na kuendeleza ushirikiano wa pande mbili, hususan katika nyanja za kiuchumi, kwa manufaa ya mataifa yote mawili.