WAZIRI CHONGOLO AWATANGAZIA NEEMA WAKULIMA WA IDOFI, KUNUFAIKA NA MRADI WA UMWAGILIAJI EKARI 1,300

WAZIRI CHONGOLO AWATANGAZIA NEEMA WAKULIMA WA IDOFI, KUNUFAIKA NA MRADI WA UMWAGILIAJI EKARI 1,300
NIRC Makambako. Waziri wa Kilimo Mhe. Daniel Chongolo ametangaza neema kwa wakulima wa Idofi, Wilaya ya Makambako, ambapo Serikai inaenda kutekeleza mradi Mkubwa wa Umwagiliaji utakaonufaisha ekari zaidi ya 1.300. Amesema, hatua hiyo itainua uchumi hivyo ni muhimu kuunga mkono mpango wa Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji wa kutekeleza mradi huo wa ujenzi wa miundombinu ya Umwagiliaji katika skimu ya Idofi, utakaowezesha kilimo chenye tija na kufungua fursa mbalimbali za maendeleo katika eneo hilo. Mhe. Chongolo amesema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi ya Idofi. Amesema, Serikali imejipanga kuhakikisha wananchi wanatumia kikamilifu rasilimali zilizopo ili kujiletea maendeleo endelevu. “Nimekuja mwenyewe kuwaambia ukweli wa kile kinachotakiwa kufanyika. Ni lazima tukae mkao wa watu tunaojua tunachokitaka,” amesisitiza Waziri Chongolo. Mheshimiwa Chongolo, amemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuwekeza fedha nyingi kati…