WATATU MBARONI KWA TUHUMA ZA MAUAJI MOROGORO Na Farida Mangube, Morogoro Jeshi la Polisi mkoani Morogoro limewakamata watuhumiwa watatu kwa tuhuma za kuhusika na matukio ya mauaji yaliyotokea katika wilaya za Malinyi, Kilombero na Kilosa. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Kamishna msaidizi wa polisi ACP Andrew Gabriel Kantimbo amesema tukio la kwanza lilitokea katika kijiji cha Nyameni, kata ya Ulaya wilayani Kilosa, ambapo mwanamke aitwaye Janeth Ernest Mazengo (52) alifariki dunia baada ya kudaiwa kushambuliwa na mumewe, Amos Zakaria Kisomeko (64). Inadaiwa kuwa chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi, ambapo mtuhumiwa alimshambulia marehemu kwa muda mrefu na kumsababishia majeraha makubwa yaliyosababisha kifo chake. Katika tukio jingine lililotokea wilayani Kilombero ambapo Ramadhani Sadick Joseph (35) anashikiliwa kwa tuhuma za kumuua Messe Germanus Ngayungwa (23) mkazi wa Ifakara, marehemu alidaiwa kupigwa na kitu kizito hadi kupoteza maisha, huku chanzo kikitajwa kuwa ni mgogoro wa ki…