Watanzania Waongoza Uwekezaji wa Ndani, Miradi 177 Yasajiliwa Robo ya Kwanza 2026

Watanzania Waongoza Uwekezaji wa Ndani, Miradi 177 Yasajiliwa Robo ya Kwanza 2026
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), Gilead Teri, a kizungumza leo Aprili 2, 2026 jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa ya hali ya uwekezaji nchini kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2026. Na Mwandishi Wetu WATANZANIA wameendelea kuongoza katika umiliki wa miradi ya uwekezaji nchini, hatua inayoonesha kuongezeka kwa mwamko wa wananchi kushiriki moja kwa moja katika shughuli za kiuchumi na maendeleo ya taifa. Akizungumza leo Aprili 2, 2026 jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa ya hali ya uwekezaji nchini kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2026, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), Gilead Teri, amesema Watanzania wanamiliki zaidi ya asilimia 57 ya miradi iliyosajiliwa ikijumuisha miradi ya wazawa na ile ya ubia kati ya Watanzania na wawekezaji wa nje. Amesema katika kipindi hicho TISEZA imesajili miradi 177 inayotarajiwa kuwekeza mtaji wa dola za Marekani milioni 1,122.09 na kuzalisha ajira …