WASIRA: KARUME AMEFANIKISHA HAKI KWA KILA WANANCHI
WASIRA: KARUME AMEFANIKISHA HAKI KWA KILA WANANCHI *Awapongeza Rais Samia, Rais Mwinyi kwa kuendeleza mafanikio Na Mwandishi Wetu, Zanziba MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, amesema kazi iliyofanywa na Muasisi wa mapinduzi na Rais wa Kwanza wa Zanzibar, hayati Sheikh Abeid Amani Karume, ndiyo inayowafanya Wazanzibari watembee kifua mbele kwa haki, uhuru na maendeleo. Aidha, amewapongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na mWenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa kuendeleza malengo ya mapinduzi na kuongoza nchi kwa haki. Wasira aliyasema hayo jana, Mjini Unguja katika kongamano la nane la kumuenzi Hayati Karume lililoandaliwa na Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere. “Madhumuni ya mapinduzi ya watu wa Zanzibar ni kukomesha upendeleo wa kiuchumi, kijamii na upendeleo wa kisheria, maana uchumi haukuwa kwa Wazanzibari wote, ardhi ilikuwa imechukuliwa na wachache na Wazanzibari watu wazima kazi yao ilikuwa kuangua nazi (wakwezi) kwa wakubwa. “Mapinduzi yakaleta mabad…