WANAWAKE 200 WAPATIWA MAFUNZO YA USIMAMIZI WA MIRATHI TEGETA
WANAWAKE 200 WAPATIWA MAFUNZO YA USIMAMIZI WA MIRATHI TEGETA
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM CHUO Kikuu Mzumbe, Ndaki ya Dar es Salaam katika kituo chake cha Tegeta, kimetoa elimu ya uelewa kwa wanawake 200 kuhusu usimamizi wa mirathi, ikiwa ni jitihada za kupunguza migogoro ya kifamilia inayotokana na masuala ya urithi. Akizungumza Aprili 1, 2026 jijini Dar es Salaam wakati wa semina hiyo, Rasi wa Chuo hicho, Prof. Cyricus Binamungu, amesema mafunzo hayo ni sehemu ya mpango endelevu wa kuwakutanisha wanajamii ili kuwajengea uelewa mpana juu ya masuala ya mirathi. Amesema usimamizi wa mirathi ni suala nyeti, huku mali nyingi zikibaki katika akaunti za mahakama zikisubiri kuchukuliwa na warithi kutokana na migogoro isiyoisha miongoni mwa familia. “Unakuta mali nyingi zipo mahakamani zinasubiri warithi, lakini migogoro inapochelewesha taratibu, mali hizo haziwafikii walengwa kwa wakati,” amesema Prof. Binamungu. Ameongeza kuwa wanaamini elimu hiyo itasaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa migogoro hiyo na kuwezesha familia kusimamia vyema urithi wa…