USHIRIKIANO WA SEKTA NI NGUZO MUHIMU KATIKA MAFANIKIO YA AFYA MOJA.

USHIRIKIANO WA SEKTA NI NGUZO MUHIMU KATIKA MAFANIKIO YA AFYA MOJA.
Mkurugenzi Msaidizi wa Afya Moja kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Dkt. Salum Manyatta, amesema kuwa Mpango Mkakati wa Afya Moja umejikita kuhakikisha wananchi wananufaika kuanzia ngazi ya  mikoa hadi taifa kupitia utekelezaji shirikishi wa sekta mbalimbali. Dkt. Manyatta ameyasema hayo Aprili 1, 2026 mkoani Morogoro wakati wa kikao kazi cha tathmini ya Mpango Mkakati wa Kitaifa wa Afya Moja 2022–2027, kilichoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Kitengo cha Afya Moja kwa kushirikiana na Shirika la CIHEB Tanzania kupitia Mradi wa Usalama wa Afya Duniani. Amesema kuwa lengo kuu la kikao hicho ni kufanya tathmini ya kina ya utekelezaji wa mpango huo kwa kuangalia shughuli zote zilizofanyika kuanzia ngazi ya uratibu kati ya taasisi mbalimbali hadi utekelezaji katika ngazi za mikoa na serikali za mitaa. “Tunachokifanya hapa ni kuainisha kwa kina utekelezaji wa Afya Moja katika sekta zote, ikiwa ni pamoja na taasisi zilizo chini ya wizara na wadau wa maen…