TRA YAPONGEZWA UTARATIBU KUFANYA KAZI SAA 24 KATIKA BOHARI YA KUHIFADHI MAFUTA

TRA YAPONGEZWA UTARATIBU KUFANYA KAZI SAA 24 KATIKA BOHARI YA KUHIFADHI MAFUTA
Na Mwandishi Wetu. MSIMAMIZI wa Bohari ya kuhifadhia Mafuta (DEPOT)ya MOIL ENERGIES Dkt. Sajad Habib Rai ameipongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kwa kuanzisha utaratibu wa kufanya kazi kwa Saa 24 katika maeneo ya bohari kwa lengo la kusaidia kuongeza ufanisi katika utoaji wao huduma. Aidha akizungumzia kuhusu upatikanaji wa mafuta katika Bohari hiyo, Dkt Sajad ambaye pia ni Meneja Mkuu wa Mansoor Industries, amesema wao kama MOIL ENERGIES wana akiba ya kutosha huku wakisubiri Meli zingine ambazo tayari zimetia nanga zishushe nishati hiyo Akizungumza siku chache mara baada ya Kamishna Mkuu wa TRA Yusuph Juma Mwenda kutembelea 'Depot' hiyo iliyopo eneo la Kigamboni Jijini Dar es Salaam, Sajad ambaye ni Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo alisema kupitia utaratibu huo kwao ni fahari kwa kuwa unarahisisha kazi. Amesema kutokana na kuongezwa huko kwa muda kwa watumishi wa TRA kuwepo katika maeneo ya kazi kama ambavyo Kamishna Mwenda amesema, shughuli zao zinakwenda kuongezeka ufanisi jambo…