TEEA YAOMBA USHIRIKIANO NA WIZARA YA MADINI KUIMARISHA UTUNZAJI WA MAZINGIRA

TEEA YAOMBA USHIRIKIANO NA WIZARA YA MADINI KUIMARISHA UTUNZAJI WA MAZINGIRA
Na mwandishi wetu, Mtumba, Dodoma Taasisi ya Wataalamu wa Mazingira Tanzania (TEEA) imeomba kushirikiana kwa karibu na Wizara ya Madini ili kuhakikisha shughuli zote za utafutaji, uchimbaji na uchakataji wa madini nchini zinafanyika kwa kuzingatia misingi ya utunzaji na uendelezaji wa mazingira. Ombi hilo limetolewa leo Aprili 1, 2026, katika ofisi za Wizara ya Madini zilizopo Mtumba jijini Dodoma, ambapo uongozi wa taasisi hiyo umefanya kikao na baadhi ya maafisa wa wizara hiyo kujadili namna bora ya kushirikiana katika kukabiliana na changamoto za kimazingira. Katika kikao hicho, viongozi wa TEEA walitaja maeneo yanayochangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira kuwa ni pamoja na uchafuzi wa vyanzo vya maji, uharibifu wa ardhi unaotokana na uchimbaji holela, ukataji wa miti bila udhibiti, pamoja na matumizi ya kemikali hatarishi kama zebaki katika shughuli za uchimbaji mdogo. Akizungumza katika kikao hicho, Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Mhandisi. Emmanuel Hanai amesema ushirikiano kat…