TANZANIA YAANGAZIA TEKNOLOJIA NA IDADI YA WATU KUKUZA MAENDELEO ENDELEVU
TANZANIA YAANGAZIA TEKNOLOJIA NA IDADI YA WATU KUKUZA MAENDELEO ENDELEVU
Na John Mapepele, New York- Marekani. Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa, amesema kuwa matumizi sahihi ya teknolojia na utafiti yana nafasi kubwa katika kushughulikia changamoto za idadi ya watu na kuharakisha maendeleo endelevu. Akizungumza katika Mkutano wa 59 wa Idadi ya Watu na Maendeleo kinachofanyika New York nchini Marekani Aprili 13-17/ 2026, Mchengerwa amesema Tanzania inaendelea kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha kuwa mabadiliko ya kiteknolojia yanawanufaisha wananchi wote. “Ni heshima kubwa kuhutubia mkutano huu kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema Mchengerwa, akisisitiza kuwa serikali inapongeza mjadala wa kimataifa unaolenga kuunganisha teknolojia, utafiti na maendeleo ya watu. Ameeleza kuwa Tanzania inatambua umuhimu wa kutumia vyema idadi kubwa ya vijana kama fursa ya kukuza uchumi. “Kutumia kikamilifu nguvu ya vijana wetu ni msingi muhimu wa kufikia ukuaji wa uchumi jumuishi na endelevu,” alisisitiza. Mheshimiwa Mchengerwa ameelez…