TAIFA GESI YAHAMASISHA MATUMIZI YA NISHATI SAFI HANDENI
TAIFA GESI YAHAMASISHA MATUMIZI YA NISHATI SAFI HANDENI
Na Oscar Assenga Kampuni ya Taifa Gesi imeendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa matumizi ya nishati safi, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuunga mkono sera ya Serikali ya kuhamasisha matumizi ya nishati rafiki kwa mazingira. Akizungumza katika tamasha lililofanyika wilayani Handeni, Mkurugenzi wa Masoko wa Taifa Gesi, Oscar Shelukindo, alisema kampuni hiyo imekuwa ikishiriki katika matamasha ya kijamii tangu mwaka jana kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi kuhusu matumizi sahihi ya gesi safi. Alisema kuwa katika tamasha hilo, wameelekeza nguvu zaidi kwa wakazi wa Handeni, hususan Kata ya Mdoe, ili kuwafikia wananchi wengi zaidi na kuwapa uelewa sahihi kuhusu faida za kutumia nishati hiyo. “Tunafurahi kuwa hapa leo kutoa elimu ya matumizi ya gesi safi, kuondoa hofu kwa wananchi na kuwahamasisha kuachana na matumizi ya nishati zisizo rafiki kwa mazingira. Pia tunatoa gesi kwa bei nafuu ili kuwavutia zaidi kuitumia,” alisema Shelukindo. Alifafanua kuwa bado kuna wananchi wengi amb…