SERIKALI YARAHISISHA UPATIKANAJI WA MITAJI KUPITIA MIKOPO NAFUU
SERIKALI YARAHISISHA UPATIKANAJI WA MITAJI KUPITIA MIKOPO NAFUU Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Deogratius Luswetula (Mb), akijibu swali la Mbunge wa Msalala, Mhe. Mabula Johnson Magangila, aliyetaka kujua wakati ambao Serikali itaanza kutumia rasilimali zake kama dhamana ili wafanyabiashara wa Kitanzania waweze kukopesheka zaidi. (Picha na Kitengo cha Mawasilino Serikalini, Wizara ya Fedha, Dodom a) Na. Josephine Majura, WF, Dodoma Serikali kupitia Wizara ya Fedha imeendelea kutekeleza mikakati ya kuimarisha uchumi wa wananchi kwa kuwezesha upatikanaji wa mitaji kupitia mikopo yenye masharti nafuu ili kuongeza uwezo wa kukopesheka kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati, sambamba na kukuza miradi ya kiuchumi inayochangia pato la Taifa. Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Deogratius Luswetula (Mb), alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Msalala, Mhe. Mabula Johnson Magangila, aliyetaka kujua lini Serikali itaanza kutumia rasilimali zake kama dhamana ili wafanyabiashara wa Kitanzania waweze kukopesheka zaidi. Mhe.…