SERIKALI YAIPONGEZA DIT KUPATA CHETI CHA ISO 21001:2018

SERIKALI YAIPONGEZA DIT KUPATA CHETI CHA ISO 21001:2018
Na Mwandishi wetu. SERIKALI imepongeza hatua ya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kwa kupata cheti cha viwango vya kimataifa cha ISO 21001:2018 kinachohusu mifumo ya usimamizi wa taasisi za elimu, hatua inayotarajiwa kuimarisha ubora wa mafunzo ya ufundi na teknolojia nchini. Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Aprili 10, 2026 kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Hussein Mohamed, amesema mafanikio hayo yanadhihirisha utekelezaji wa maono ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ya kuimarisha elimu yenye ujuzi, ubunifu na tija kwa maendeleo ya uchumi wa taifa. Amesema Serikali imeendelea kufanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya elimu ili kuhakikisha vijana wanapata ujuzi unaoendana na mahitaji ya soko la ajira na viwanda. “Mheshimiwa Rais amekuwa akisisitiza kuwa hatuhitaji elimu ya vyeti pekee, bali elimu yenye ujuzi, ubunifu na tija. Kupitia uwekezaji huu mkubwa, vijana w…