POLISI YAJIDHATITI KUHAKIKISHA USALAMA NA UTULIVU WAKATI WOTE WA SIKUKUU ZA PASAKA
POLISI YAJIDHATITI KUHAKIKISHA USALAMA NA UTULIVU WAKATI WOTE WA SIKUKUU ZA PASAKA
Na mwandishi wetu Jeshi la Polisi nchini Tanzania limesema limejipanga vyema kuanzia ngazi ya Kata na kwa kushirikiana na Kamati za ulinzi na usalama kuhakikisha kuwa usalama na utulivu unadumishwa wakati wote wa kipindi cha kuhitimisha mfungo wa Kwaresma na sikukuu za pasaka kwa waumini wa dini ya Kikristo wakati wote wa ibada Kanisani na majumbani mwao. Taarifa ya Msemaji wa Jeshi la Polisi Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) David Misime kuhusu kuimarishwa kwa hali ya usalama kuelekea sikukuu za Pasaka iliyotolewa leo Alhamisi Machi 02, 2026 kwa Vyombo vya habari, imetoa wito pia kwa kila mmoja wakati wa ibada na sherehe za pasaka kuhakikisha makazi yanakuwa chini ya uangalizi badala ya kuacha makazi yao bila ya usimamizi. "Aidha kama tutaruhusu watoto wetu kutoka kwaajili ya kwenda kusherehekea sikukuu hizi katika maeneo stahiki na salama, kila mmoja ahakikishe wanakuwa na uangalizi wa mtu mzima na mwenye akili timamu. Pia tunatoa wito kwa kila mmoja kuzingatia sheria, kanuni na isha…