NISHATI SAFI YAFUNGUA MILANGO YA FURSA KWA WATENGENEZA MAUDHUI

NISHATI SAFI YAFUNGUA MILANGO YA FURSA KWA WATENGENEZA MAUDHUI
Na Mwandishi Wetu, Mwanza Watengeneza maudhui nchini wamehamasishwa kutumia ubunifu wao kujipatia kipato kupitia fursa zitokanazo na nishati safi ya kupikia, kwa kuelimisha jamii kupitia kazi zao zikiwemo video za elimu, vichekesho, hadithi na kampeni mbalimbali zitakazowafikia wananchi kwa urahisi. Wito huo umetolewa Aprili 1, 2026 jijini Mwanza na Mhandisi Nishati kutoka Wizara ya Nishati, Benezeth Kabunduguru, wakati akizungumza katika mafunzo kwa watengeneza maudhui (content creators).  Mafunzo hayo yameandaliwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania, huku Wizara ya Nishati ikiwa miongoni mwa wawezeshaji wakuu. Amesema mafunzo hayo yamelenga kuwasaidia watengeneza maudhui kuboresha kazi zao kwa kuzingatia mbinu za kubiasharisha maudhui mtandaoni, kujenga chapa binafsi pamoja na kuzingatia masuala ya hakimiliki. Kabunduguru ameeleza kuwa watengeneza maudhui wana nafasi kubwa ya kubadilisha mtazamo wa jamii kupitia ubunif…