NEMC YAIMARISHA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA KATIKA USIMAMIZI WA MAZINGIRA UTURUKI
NEMC YAIMARISHA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA KATIKA USIMAMIZI WA MAZINGIRA UTURUKI
- Yabadilishana uzoefu katika masuala mazima ya Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira . Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limekutana na kufanya mazungumzo na Wizara ya Mazingira, Maendeleo ya Miji na Mabadiliko ya Tabianchi, Taasisi ya Utafiti wa Udongo, Maji na Majanga, Idara ya Maji safi na Maji Taka, Taasisi ya Mradi wa Maendeleo ya Mji wa Konya na Kampuni ya Turko wakati wa maonesho ya zana bora na pembejeo za kilimo na kilimo hifadhi katika Mji wa Konya nchini Uturuki Mazungumzo hayo yalilenga kubadilishana uzoefu katika masuala ya usimamizi na uhifadhi wa mazingira ikiwa ni pamoja na kuimarisha ushirikiano wa Kimataifa na kujifunza mbinu bora zinazotumika katika kukabiliana na changamoto za kimazingira. Akifafanua utekelezaji wa majukumu kutoka NEMC,wakati wa mazungumzo hayo Afisa Ustawi wa Jamii Mwandamizi Bi Suzan Chawe amesema wajibu wa Baraza ni kushauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu masuala ya Mazingira na kusimamia Uhifadhi wa Maz…