MWALIMU AUWAWA KIKATILI KWA TUHUMA ZA IMANI POTOFU SUMBAWANGA
Jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa limewakamata watuhumiwa (25) kwa tuhuma za kuhusika katika tukio la mauaji ya Henry Shubati Myuwanga (50), Mwalimu wa Shule ya Msingi Wema Mkoani Songwe. Tukio hilo la mauaji lilitokea tarehe 04 Aprili, 2026 majira ya saa 02:30 usiku katika Kijiji cha Kilyamatundu, Wilaya ya Sumbawanga. Marehemu alifika kijijini hapo siku hiyo akitokea Mlowo, Mkoa wa Songwe kwa lengo la kuuza sabuni za maji anazozitengeneza, biashara ambayo amekuwa akiifanya mara kwa mara kijijini hapo anapokuwa na muda wa kufanya hivyo. Chanzo cha tukio hilo kilitokana na kutokukubaliana bei ya sabuni kati ya mwalimu (marehemu) na kijana mmoja muuza duka kijijini hapo aitwaye Cleuben Simchimba ambaye amekimbia tunaendelea kumtafuta. Kufuatia hali hiyo, kijana huyo aliamua kufanya kitendo kiovu cha kupiga kelele na kumtuhumu marehemu kuwa amemshika begani na kwamba nyeti zake zimepotea. Kutokana na kelele za kijana huyo, wananchi walikusanyika na kuanza kumshambulia mwalimu huyo kwa kumpiga…