Mradi wa CERA kutafiti mbegu za Mpunga unaohimili Mabadiliko ya tabianchi Afrika.
Mradi wa CERA kutafiti mbegu za Mpunga unaohimili Mabadiliko ya tabianchi Afrika.
Na: Calvin Gwabara – Morogoro. Wakulima wa kilimo cha mpunga
kinachotegemea mvua nchini wamewashukuru watafiti wa Mradi wa Mpunga Himilivu
kwa Mabadiliko ya Tabianchi na Rafiki kwa Mazingira barani Afrika (CERA) kwa
jitihada walizozianzisha kuzalisha mbegu bora ya mpunga unaohimili changamoto
za hali ya hewa ili kuinua kipato cha wakulima wa zao hilo Afrika. Hayo yamebainishwa na wakulima
kutoka mikoa ya Morogoro, Shinyanga na Songwe wakati wa zoezi la ukusanyaji wa
takwimu za awali na taarifa mbalimbali muhimu zitakazosaidia watafiti hao
kuweza kujua changamoto wanazokabiliana nazo katika kilimo hicho ili kuweza
kusaidia wao kuzalisha mbegu mpya zilizoboreshwa ambazo zitaweza kuhimili
mabadiliko hayo ya tabia nchi. Ukusanyaji huo wa takwimu
umefanyika kwa ushirikiano kati ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) na Taasisi
ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), katika vijiji nane ukishirikisha wakulima
wapatao 258. Akizungumza na watafiti hao mkulima
Bwana Maroja Shana kutoka Kijiji ch…