MKONGO WA TAIFA WA MAWASILIANO WAFIKIA WILAYA 121 KATI YA 139

MKONGO WA TAIFA WA MAWASILIANO WAFIKIA WILAYA 121 KATI YA 139
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amezindua rasmi maunganisho ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika wilaya 85 pamoja TTCLkukabidhiwa Mkongo wa Mawasiliano iliokuwa ukiendeshwa na Umoja wa Watoa Huduma za Mawasiliano (Yas, Vodacom, Airtel). Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mheshimiwa Rais amesema Mkongo wa Taifa ni muhimili muhimu wa uchumi na usatwi wetu wa Taifa letu, na nguzo ya ulinzi na usalama wa nchi. Ameitaka TTCL kuhakikisha miundombinu hiyo inalindwa na kudumishwa kwa manufaa ya Taifa. Kwa sasa, Mkongo wa Taifa umefikia urefu wa kilomita 15,167, ukiunganisha mikoa yote na kufika katika wilaya 121 kati ya 139 za Tanzania Bara. Aidha, wilaya 18 zilizosalia zitaunganishwa kwenye Mkongo wa Taifa ifikapo Desemba 2026, sambamba na kukamilisha na mradi wa kuunganisha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ifikapo Aprili 2027. Mradi huu una mchango mkubwa katika kukuza TEHAMA nchini, kuchochea ukuaji wa uchumi, na kuboresha utoaji wa huduma kwa wanan…