MAKOYE NA KISAKA WAKAMATWA KWA KUZUSHA ‘WAMEPOTEZA SEHEMU ZA SIRI’ KAHAMA
MAKOYE NA KISAKA WAKAMATWA KWA KUZUSHA ‘WAMEPOTEZA SEHEMU ZA SIRI’ KAHAMA
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, SACP Janeth Magomi Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limewakamata watuhumiwa wawili ( Kisaka Elinihaki na Makoye James) kwa tuhuma za kusambaza taarifa za uongo kuhusu kupoteza sehemu zao za siri, hali iliyosababisha taharuki kubwa miongoni mwa wananchi katika Wilaya ya Kahama. Taarifa hiyo imetolewa leo Aprili 7, 2026 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, SACP Janeth Magomi, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake. Kamanda Magomi amesema tukio la kwanza lilitokea Aprili 4, 2026 katika Soko Kuu lililopo eneo la Stendi Kuu ya Mabasi, Kata ya Kahama Mjini, ambapo mwaume mmoja aitwaye Kisaka Elinihaki (22), mkazi wa Majengo, alidai kupoteza sehemu zake za siri kimiujiza baada ya kuguswa bega la kushoto na dereva mmoja aitwaye Joseph Godfrey (36), mkazi wa Shunu. Amesema taarifa hiyo ya uongo ilisababisha taharuki kubwa kwa wananchi waliokuwepo eneo hilo, ambapo baadhi yao walichukua sheria mkononi na k…