MAELFU YA WANANCHI WAJITOKEZA KUMZIKA KAKA MKUBWA WA MKE WA MBUNGE WA JIMBO LA KIBAHA MJI
NA VICTOR MASANGU, DAR ES SALAAM Maelfu ya wananchi mbali mbali wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi wa dini, taasisi na mashirika binafsi ,mashabiki wa soka na mziki wa dansi pamoja na wananchi mbali mbali …. wamejitokeza kwa wingi katika makaburi ya Kinonddoni Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuhudhuria mazishi ya mfanyabiashara maarufu na mshabiki mkubwa wa klabu ya soka ya Simba Emmanuel Nderimo almaarufu Macha ambaye alifariki dunia machi 30 mwaka huu. Katika mazishi hayo ambayo yalihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa serikali pamoja na chama cha mapinduzi (CCM) yalikubikwa na vilio na majonzi makubwa ambayo yalipelekea baadhi ya watu kushindwa kujizuia kwa kutokwa na machozi wakati wa zoezi la kuuga mwili huo. Moja kati ya viongozi maarufu ambao walihudhulia katika msiba huo ni Mwenyekiti wa klabu ya soka ya Simba Murtaza Mangungu pamoja ambapo aliambatana na viongozi wengine mbali mbali wa klabu hiyo ambapo amesema marehemu Emmanuel alikuwa na mchango mkubwa sana …