MADEREVA VIP POLISI WATAKIWA KUIMARISHA ULINZI, KUEPUKA AJALI
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM Madereva wa viongozi mashuhuri (VIP) wa Jeshi la Polisi wametakiwa kuweka mbele jukumu lao la msingi la kulinda maisha ya viongozi wanaowaendesha kwa kuzingatia tahadhari na kuzuia ajali zinazoweza kuepukika, ili kulinda rasilimali watu muhimu kwa taifa. Wito huo umetolewa na Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Dkt. Prosper Mgaya, wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya mwezi mmoja kwa madereva wa viongozi hao yanayofanyika chuoni hapo. Dkt. Mgaya amesema madereva wa VIP wanapaswa kufanya kazi kwa weledi, umakini na nidhamu ya hali ya juu, akisisitiza kuwa viongozi wa juu huandaliwa kwa muda mrefu kwa ajili ya kulitumikia taifa, hivyo kupoteza maisha yao kutokana na uzembe wa madereva ni hasara kubwa kwa nchi. Aidha, amewahimiza washiriki wa mafunzo hayo kuyachukulia kwa uzito ili yawaletee mabadiliko chanya na kuwasaidia kupanda madaraja kutoka ngazi za chini hadi za juu. Kwa upande wake, Mkuu wa Usafirishaji Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, SACP Fort…