JKCI KINARA AFRIKA MASHARIKI, YAFANYA UPASUAJI ZAIDI YA 3,000 WA MOYO KWA MWAKA

JKCI KINARA AFRIKA MASHARIKI, YAFANYA UPASUAJI ZAIDI YA 3,000 WA MOYO KWA MWAKA
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akiongea na Waandishi wa Habari kuhusu Miradi ya Maendeleo na Fursa za Vijana kwa Mwaka 2025/26 katika Ukumbi wa Habari MAELEZO ulipo Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Jijini Dodoma. Na. Meleka Kulwa- Fullshangwe Blog, Dodoma  Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imeendelea kuongoza katika utoaji wa huduma za matibabu ya moyo katika ukanda wa Afrika Mashariki na Jangwa la Sahara, ikifanya zaidi ya upasuaji 3,000 wa tundu dogo kwa mwaka. Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Dkt. Peter Kisenge, amesema kuwa mafanikio hayo yametokana na uwekezaji mkubwa wa Serikali katika sekta ya afya pamoja na kuimarika kwa rasilimali watu, vifaa tiba na miundombinu ya kisasa. ameyabainisha hayo Aprili 9,2026, alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dodoma, Aidha, Dkt. Kisenge amesema kuwa JKCI iliyoanzishwa mwaka 2015 kwa ajili ya kutoa huduma za kibingwa bobezi, kufanya tafiti na kutoa mafunzo, imef…