DKT MWIGULU: TUNATAMBUA MCHANGO WA WAFANYAKAZI

DKT MWIGULU: TUNATAMBUA MCHANGO WA WAFANYAKAZI
WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango wa wafanyakazi wa sekta ya umma na sekta binafsi katika kukuza uchumi na maendeleo ya Taifa. Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu ameyasema hayo jana jioni Aprili 13, 2026 jijini Dodoma katika Hafla ya Maandalizi ya Mei Mosi, 2026 ambayo Kitaifa inafanyika mkoani Njombe. Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amesema Serikali inaendelea kuwaenzi wafanyakazi nchini kutokana na umuhimu wao mkubwa kwa Taifa. Katika hafla hiyo ya awali, kiashi cha shilingi bilioni 1.105 kimekusanywa ambapo Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu alisema fedha hizo zitausaidia mkoa mwenyeji kukamilisha shughuli za maandalizi kwa ajili ya tukio hilo. Mheshimiwa Waziri Mkuu aliongeza kwa kulipongeza Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA) kwa ubunifu wa kuhakikisha maadhimisho ya Mei Mosi yanaacha alama katika mkoa mwenyeji. “Wenzetu TUCTA wamekuja na ubunifu kwamba shughuli za Mei Mosi zinaacha alama katika mkoa husika kwa kutekeleza miradi mbalimbali kama walivy…