DKT. GWAJIMA ATOA WITO KWA JAMII NA WAZAZI KUSHIRIKI MALEZI YA WATOTO KIKAMILIFU

DKT. GWAJIMA ATOA WITO KWA JAMII NA WAZAZI KUSHIRIKI MALEZI YA WATOTO KIKAMILIFU
Na Saidi Saidi WMJJWM - Dodoma Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe.Dkt. Dorothy Gwajima, ametoa wito kwa jamii na wazazi kushiriki kikamilifu katika malezi na ulinzi wa watoto, ili kuzuia ongezeko la watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani. Akizungumza na waandishi wa habari Aprili 01, 2026 jijini Dodoma kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto anayeishi na kufanya kazi mtaani, yatakayofanyika Aprili 12, 2026 Jijini Dar Es Salaam yakiwa na Kaulimbiu isemayo “Malezi na Ulinzi wa Mtoto, Wajibu wetu Sote”. Amesema ushiriki wa pamoja ni muhimu ili kuhakikisha watoto wanakua katika mazingira salama na yenye maadili mema huku akisisitiza jukumu la malezi si la wazazi pekee, bali ni la jamii nzima. Aidha, Waziri Gwajima ameeleza kuwa changamoto kama umasikini, migogoro ya kifamilia, na ukatili dhidi ya watoto zimekuwa zikichangia watoto wengi kukimbilia mitaani. Ameibainisha pia mafanikio ya juhudi za Serikali katika kuwaokoa watoto wa mitaani kuwa …