DKT AKWILAPO KUSHIRIKI KONGAMANO LA MIJI AFRIKA NAIROBI
DKT AKWILAPO KUSHIRIKI KONGAMANO LA MIJI AFRIKA NAIROBI
Na Munir Shemweta, Nairobi Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Leonard Akwilapo, anatarajiwa kuongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki Kongamano la Pili la Jukwaa la Miji Afrika (2nd African Urban Forum) litakalofanyika kuanzia tarehe 8 hadi 10 Aprili 2026 katika jiji la Nairobi nchini Kenya. Kongamano hilo linaongozwa na kauli mbiu isemayo “Adequate Housing for All: Advancing Socio-Economic and Environmental Transformation Towards the Realization of Agenda 2063,” linalenga kuhamasisha mijadala itakayotoa fursa kwa washiriki kutoka nchi mbalimbali za Afrika kubadilishana uzoefu na suluhisho bunifu katika kukabiliana na changamoto za maendeleo ya miji na makazi. Kupitia kongamano hilo, Tanzania inatarajiwa kutoa tamko la nchi litakaloeleza jitihada za Serikali katika kuchochea maendeleo endelevu ya miji na makazi, ikiwa ni pamoja na sera, mipango na mikakati inayotekelezwa kuboresha makazi na upangaji wa miji. Aidha, Mhe. Dkt Akwilapo atashiriki katika mijadala ya ngazi y…