DC MPOGOLO AWAPONGEZA VIONGOZI WA DINI KWA KUIMARISHA AMANI NA MAENDELEO

DC MPOGOLO AWAPONGEZA VIONGOZI WA DINI KWA KUIMARISHA AMANI NA MAENDELEO
Mkuu wa wilaya ya Ilala, Mheshimiwa Edward Mpogolo, ambaye amemuwakilisha Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Albert Chalamila, amepongeza na kuwashukuru viongozi wa dini kwa mchango wao mkubwa wa kuimarisha na kudumisha amani lengo kuleta maendeleo katika jamii. Akizungumza katika maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 19 ya kanisa la WRC Kivule tarehe,6 April, DC Mpogolo alisema licha ya changamoto mbalimbali viongozi wa dini wameendelea kujitoa na kushirikiana na serikali pale wanapohitajika. Aidha alimpongeza mgeni rasmi, Deus Sangu, Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu kazi na ajira , ambaye alimuwakilisha makamu wa raisi Mheshimiwa Emmanuel Nchimbi kwa kushiriki katika maadhimisho hayo. DC Mpongolo ameipongeza serikali chini ya Mheshimiwa raisi Dkt Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake za kuleta maendeleo kwa utoaji wa fedha katika mkoa huo na kusisitiza kuwa mafanikio hayo yasingewezekana bila uwepo wa amani, maadili na mchango wa viongozi wa dini. Aliongeza kuwa viongozi wa dini wam…