DAR ES SALAAM KUPOKEA MWENGE WA UHURU APRIL 13, 2026

DAR ES SALAAM KUPOKEA MWENGE WA UHURU APRIL 13, 2026
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila amewataka wananchi wa Mkoa huo kujitokeza katika mbio za Mwenge wa Uhuru unaotarajia kuwasili jijini humo aprili 13 mwaka huu ukitokea Mkoa wa Kaskazini Unguja ambapo utakimbizwa umbali wa kilometa 392.22 kwenye Wilaya zote tano za mkoa huo ukikagua, kuzimdua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi 35 yenye thamani ya shilingi bilioni 113.5 Akizungumza na waandishi wa habari RC Chalamila amesema shabaha ya mbio za mwenge wa uhuru ni kuleta umoja, mshikamano na udugu baina ya watanzania ambapo amesema aprili 13 baada ya kuwasili utakimbizwa wilayani Ilala, April 14 wilaya ya Kigamboni, April 15 wilaya ya Temeke, April 16 wilaya ya Ubungo na April 17 wilaya ya Kinondoni na April 18 Mkoa utakabidhi Mkoa wa Pwani. RC Chalamila amesema Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu wa 2026 umebeba ujumbe wa kudumisha amani, umoja na mshikamano wa kitaifa chini ya kauli mbiu isemayo "Tanzania ni Yetu Sote, Tushikamane kwa Pamoja Kuleta Maendeleo" Sanj…