CRDB YAWAPA DILI NONO WATEJA: WASHINDI KUSAFIRI MAREKANI KUSHUHUDIA KOMBE LA DUNIA 2026
CRDB YAWAPA DILI NONO WATEJA: WASHINDI KUSAFIRI MAREKANI KUSHUHUDIA KOMBE LA DUNIA 2026
Benki ya CRDB imeendelea kuwazawadia wateja wake kwa zawadi nono kupitia promosheni maalum ya matumizi ya kadi ya TemboCard Visa, huku zawadi kubwa ikiwa ni safari ya kwenda Marekani kushuhudia fainali za Kombe la Dunia 2026. Zawadi hizo zimekabidhiwa Aprili 14, 2026 katika hafla iliyofanyika makao makuu ya benki hiyo yaliyopo Upanga, jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kuhamasisha matumizi ya mifumo ya malipo ya kidijitali nchini. Kupitia kampeni hiyo, wateja wanahimizwa kutumia TemboCard Visa katika malipo yao ya kila siku kupitia mashine za POS au mtandaoni, ambapo kila muamala unaongeza nafasi ya kushiriki katika droo mbalimbali za ushindi. Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja Mwandamizi wa Kitengo cha Kadi (Card), Karington Chahe, amesema lengo la kampeni hiyo ni kuwapa wateja fursa ya kipekee ya kushinda zawadi kubwa huku wakinufaika na huduma salama, rahisi na za kisasa. Ameeleza kuwa droo ya kwanza tayari imefanyika na kutoa washindi kadhaa waliopata zawadi m…