CCM YAPONGEZA KASI YA UJENZI BARABARA YA LAMI KAHAMA - KAKOLA UNAOFADHILIWA NA MIGODI YA BARRICK NCHINI

CCM YAPONGEZA KASI YA UJENZI BARABARA YA LAMI KAHAMA - KAKOLA UNAOFADHILIWA NA MIGODI YA BARRICK NCHINI
Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi ya (CCM) wilayani Kahama mkoani Shinyanga, imepongeza kasi ya Ujenzi wa Barabara ya Kahama-Kakola yenye urefu wa Kilomita 73 Inayojengwa kwa kiwango cha lami kwa Ufadhili Migodi ya Barrick nchini ya Bulyanhulu na North Mara itakayogharimu kiasi cha shilingi bilioni 101.2.Ujenzi wa barabara hii unatekelezwa kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation. Ujumbe wa kamati ya siasa wilaya ya Kahama ukiongozwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama Thomas Myonga ulitembelea mradi huo wa ujenzi wa barabara na kutoa pongezi kwa kampuni ya Barrick nchini yenye ubia na Serikali ya Tanzania kupitia kampuni ya Twiga Minerals kwa kufanya uwekezaji unaoenda sambmba na kufanikisha miradi mikubwa endelevu inayobadilisha maisha ya wananchi kuwa bora ma itakayoacha alama ya kudumu hata kwa vizazi vijavyo. Thomas Myonga Akiongea wakati wa ziara hiyo Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama Thomas Myonga amesema wamefurahishwa kuona mradi huu mkubwa unaendelea …