BALOZI KOMBO AKUTANA NA WANAFUNZI MAURITIUS, AWATAKA KUWA MABALOZI WEMA WA TANZANIA
BALOZI KOMBO AKUTANA NA WANAFUNZI MAURITIUS, AWATAKA KUWA MABALOZI WEMA WA TANZANIA Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kombo, alikutana na kuzungumza na wanafunzi wa Kitanzania wanaosoma nchini Mauritius katika Chuo Kikuu cha Middlesex Aprili 13,2026, na kuwashauri wanafunzi hao kuhusu maisha yao ya masomo pamoja na wajibu wao wa kuiwakilisha Tanzania wakiwa ugenini. Katika mazungumzo hayo, Waziri Kombo, ambaye aliambatana na Balozi wa Tanzania nchini Mauritius mwenye makazi yake Harare, Zimbabwe, aliwahimiza wanafunzi hao kuwa mabalozi wazuri wa nchi yao na kuzingatia maadili mema ya Kitanzania, nidhamu, na mwenendo unaoendana na heshima ya taifa. Alisisitiza umuhimu wa kuitangaza Tanzania vyema popote walipo na kuepuka kuwaangusha wazazi wao waliowezesha safari yao ya elimu na kueleza kuwa juhudi zao zinapaswa kuonekana si tu kitaaluma bali pia kitabia. “Ninyi ni mabalozi wa taifa lenu, hivyo muiwakilishe vyema nchi yenu na msiwaangushe wazazi wenu. Nimezungumza na Mkuu wa Chuo, amenihakikishia kuwa wanafunzi wa Tanzania mnafanya vizuri …