ASKOFU MKUU MULENGA ATOA WITO MKALI KWA VIONGOZI WA DINI: “HUBIRINI AMANI, SIYO UCHONGANISHI”
ASKOFU MKUU MULENGA ATOA WITO MKALI KWA VIONGOZI WA DINI: “HUBIRINI AMANI, SIYO UCHONGANISHI”
Na Hadija Bagasha - Tanga Viongozi wa dini kote nchini wakiwemo Maaskofu wametakiwa kuhakikisha wanatumia majukwaa yao ya kidini kuhubiri masuala ya amani, upendo na mshikamano badala ya kuhubiri mambo yanayoleta uchonganishi yanayoweza kugawa jamii na kutengeneza chuki miongoni mwao. Hayo yamesemwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la The Free Pentecostal Church of Tanzania (FPCT), Tanzania Stivie Mulenga wakati wa ibada maalum ya Pasaka iliyofanyika kanisani hapo jijini Tanga. Amesema kuwa ibada zinapaswa kubaki kuwa mahali pa kumtukuza Mungu, siyo jukwaa la kuwashambulia au kuwapendelea watu fulani. Katika mahubiri yake yaliyojaa msisitizo wa maadili na mshikamano wa kijamii, alikumbusha kuwa msingi wa imani ya Kikristo ni amani, siyo migawanyiko. Ameeleza kuwa Yesu Kristo hakuja duniani kuleta chuki au uchonganishi, bali alikuja kuleta upendo na amani miongoni mwa wanadamu. Aidha, amesema kuwa kufufuka kwake ni ishara ya ushindi wa amani juu ya giza, hivyo viongozi wa dini wanapaswa kuendel…