WIZARA YA ARDHI YAWASILISHA RANDAMA YA BAJETI 2026/2027 KWA KAMATI YA BUNGE

WIZARA YA ARDHI YAWASILISHA RANDAMA YA BAJETI 2026/2027 KWA KAMATI YA BUNGE
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo akizungumza wakati wa kuwasilisha Randama ya Wizara yake kwa mwaka wa fedha 2026/2026 mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii tarehe 23 Machi 2026 jijini Dodoma. Kushoto ni Naibu Waziri wa Ardhi Mhe. Kaspar Mmuya na kulia ni Katibu Mkuu Mhandisi Anthony Sanga . Na  Munir Shemweta, WANMM Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imewasilisha Randama ya Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027 mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Bajeti kuu ya Serikali. Akiwasilisha randama hiyo leo tarehe 23 Machi, 2026 jijini Dodoma, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo amesema wizara yake imejipanga kuendelea kutekeleza vipaumbele muhimu vinavyolenga kuboresha sekta ya ardhi, ikiwa ni pamoja na kuongeza kasi ya upimaji wa ardhi, utoaji wa hati miliki, pamoja na kudhibiti migogoro ya ardhi nchini. Ameongeza kuwa, k…