WAZIRI MUDRIK SORAGA AZUNGUMZA NA WAANDISHI MAELEZO ZANZIBAR.
WAZIRI MUDRIK SORAGA AZUNGUMZA NA WAANDISHI MAELEZO ZANZIBAR.
Waziri wa Mawasiliano Teknolojia ya Habari na Ubunifu Mudrik Ramadhan Soraga akijibu Maswali ya Waandishi wa Habari katika Mkutano na Waandishi hao akielezea Maendeleo na Mafanikio yaliopatikana katika Wiazara kufikia Siku Mia Moja za Uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk,Hussein Ali Mwinyi kwa kipindi chake cha Pili hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Habari Maelezo Rahaleo Zanzibar. Na Maelezo Zanzibar 23.03.2026 Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeanzisha mfumo wa kidijitali unaowezesha Wizara na Taasisi kusimamia na kuweka taarifa za huduma za Serikali kidijitali (Zanzibar Government Services Directory - ZGSD) ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma. Akizungumza katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar wakati akizungumza na waandishi wa habari katika siku 100 za Mafanikio za Uongozi wa Dk. Mwinyi, Wazir wa Mawasiliano, Teknolojia ya habari na Ubunifu Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga amesema Serikali imeimarisha upatikanaji na matumizi ya teknol…