WAZIRI MKUU AONGOZA WAOMBOLEZAJI MAZISHI YA WILLIAM LUKUVI
WAZIRI MKUU AONGOZA WAOMBOLEZAJI MAZISHI YA WILLIAM LUKUVI
Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba, amesema aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) na Mbunge wa Isimani, William Lukuvi, ataendelea kukumbukwa na Watanzania kwa mchango wake mkubwa na utumishi uliotukuka katika nafasi mbalimbali alizowahi kushika. Akizungumza katika ibada ya mazishi iliyofanyika nyumbani kwa marehemu katika kijiji cha Idodi, wilayani Iringa mkoani Iringa leo Jumanne, Machi 31, 2026, Waziri Mkuu alisema kuwa Lukuvi alikuwa nguzo muhimu katika kuleta maendeleo kupitia nafasi zake serikalini, bungeni na ndani ya chama. “Mheshimiwa Lukuvi atakumbukwa kwa mengi na Watanzania kutokana na utumishi wake uliotukuka katika nafasi mbalimbali. Mchango wake kwa jamii na Watanzania kwa ujumla umekuwa chachu ya maendeleo,” alisema. Waziri Mkuu ambaye aliongoza mazishi hayo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, aliwahakikishia wananchi kuwa ndoto na maono ya marehemu yataendelea kutekelezwa. “Kwa niaba ya Mhesh…