WAVUVI ACHENI KUPUUZA MATUMIZI YA VIFAA OKOZI-DC HAULE
WAVUVI ACHENI KUPUUZA MATUMIZI YA VIFAA OKOZI-DC HAULE
Mkuu wa Wilaya ya Rorya Dkt. Khalfany Haule akizungumza na maafisa wa TASAC waliotembelea Ofisi ya Mkoa wa Mara hawapo pichani. Afisa Mfawidhi wa TASAC mkoa wa Mara Mhandisi Hezron Lusangija akitoa elimu ya usalama majinI kwa Wavuvi wa Wilaya ya Rorya. *Jaketi Okozi ni Uhai na sio mzigo kwa msafirishaji Na Mwandishi Wetu SERIKALI ya Wilaya ya Rorya imetoa wito kwa wavuvi na wamiliki wa mitumbwi kuacha kupuuza matumizi ya vifaa vya kuokoa maisha majini. Hayo ameyasema Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Mhe. Dkt. Khalfany Haule wakati maafisa Shirika la Uwakala wa Meli (TASAC) walipotembelea Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwa ajili ya kutoa elimu ya Usalama wa vyombo vya majini. Dkt. Haule alionya dhidi ya mtazamo potofu kwamba maboya ni mzigo wa gharama na kikwazo cha kazi ya uvuvi Amesema kwa takwimu za mwaka uliopita, zaidi ya wavuvi 20 walipoteza maisha kutokana na mitumbwi kuzama, licha ya kuwa na maboya ndani ya vyombo lakini bila kuyavaa. "Kupoteza maisha ni pigo kubwa kwa familia na inapunguza…