WATU WENYE ULEMAVU WASISITIZWA KUCHANGAMKIA MIKOPO YA ASILIMIA 10

Katibu mstaafu wa Chama cha watu wenye ulemavu wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma Angelus Milinga,akizungumza jana kuhusu mikopo ya asilimia kumi inayotolewa na Serikali kupitia Halmashauri za wilaya ambapo amewataka walemavu wenye kuhitaji mikopo hiyo kwenda kwenye Halmashauri zao kwa ajili ya kupata utaratibu wa mikopo hiyo. Na Muhidin Amri, Songea WATU wenye ulemavu mkoani Ruvuma,wametakiwa kuunda vikundi vitakavyowapa sifa ya kunufaika na uwezeshaji wenye lengo la kuwajengea uwezo wa kiuchumi na hatimaye kuondokana na umaskini. Wameonywa juu ya tabia ya kukaa barabarani na kuzunguka kwenye maeneo ya starehe kwa ajili ya kuomba misaada badala yake wajitokeze kwenda Halmashauri kuchukua mikopo inayotolewa bila riba kutoka asilimia mbili ya mapato ya ndani ili waweze kujipatia kipato na kuondokana na umaskini. Wito huo umetolewa jana na Mwanzilishi wa Chama cha walemavu wilayani Songea Angelus Milinga,wakati akizungumzia kuhusu mikopo ya asilimia kumi inayotolewa na Halmashauri za wilaya kuto…