Watoto Kushiriki Mbio za Km 2, Viwango Vipya Vyalenga Usalama Run 4 Autism 2026
Watoto Kushiriki Mbio za Km 2, Viwango Vipya Vyalenga Usalama Run 4 Autism 2026 Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam. Waandaaji wa mbio za Run 4 Autism Tanzania Half Marathon 2026 wameweka wazi muongozo mpya wa ushiriki utakaozingatia makundi ya umri na viwango vya umbali, hatua inayolenga kulinda usalama wa washiriki na kuendana na kanuni mpya za riadha zilizoanza kutumika nchini kuanzia Januari 2026. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Lukiza Autism Sports Foundation, mbio za watoto pamoja na watu wenye ulemavu hazitazidi kilomita mbili (km 2), kufuatia maelekezo ya kitaifa yanayokataza watoto kushiriki umbali mrefu zaidi ya huo. Kundi hilo linalenga zaidi watoto wenye umri chini ya miaka 12, huku watu wazima wanaoruhusiwa kushiriki katika mbio hizo wakiwa ni wale wanaoambatana na watoto wadogo. Aidha, watoto wenye umri kati ya miaka 13 hadi 17 watashiriki mbio za kilomita tano (km 5), wakati washiriki wenye umri wa miaka 18 na kuendelea watakimbia mbio za kilomita 10 pamoja na nusu marathon ya kilomita 21.1. Mbio hizo zinatarajiwa kufanyika Aprili 4, 2026 katika viwa…