WATATU WANASHIKILIWA NA POLISI KWA KUCHAKACHUA MBOLEA MAKAMBAKO

WATATU WANASHIKILIWA NA POLISI KWA KUCHAKACHUA MBOLEA MAKAMBAKO
Polisi mkoani Njombe inawashikilia watu watu akiwemo James Elias Nziku(41),Ahmed Abdalah Gunda(21)na Seleman Lameck Msiani(37) wakazi wa makambako mkoani Njombe baada ya kukutwa katika ghara la mfanyabiashara wa pemebejeo anaejulikana kwa jina la Ayoub Sanga wakichakachua mbolea za kampuni ya INTRACOM Kwenda kwenye mifuko ya mbolea za DAP zinazosambazwa na kampuni ya mbolea ya taifa TFC ili kuwauzia wakulima na kujitengenea faida zaidi. Akitoa ufafanuzi kuhusu kushikiliwa kwa watu watatu waliokuwa wakifanya kazi ya kuchakachua mbolea katika ghara la mfanyabiashara wa pembejeo Makambako Ayoub Sanga ,kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Mahamoud Banga amesema watu watatu wamekamatwa wakiwa na mifuko 188 ya mbolea iliyochakachuliwa ,mashine ya kufungia mifuko na mifuko mitupu ya makampuni tofauti,hivyo wanaendelea na msako ili wahusika wote wafikishe katika vyombo vya sheria. Betrice Tarimo ambae ni afisa Kilimo halmashauri ya mji wa Makambako na Samwel Msongwe msimamizi wa kampuni ya TFC kand…