WANANCHI SHINYANGA WATOA MAONI RASIMU YA MKATABA WA HUDUMA ZA SHUWASA, WAPENDEKEZA MITA ZA PRE -PAID
WANANCHI SHINYANGA WATOA MAONI RASIMU YA MKATABA WA HUDUMA ZA SHUWASA, WAPENDEKEZA MITA ZA PRE -PAID
Mkurugenzi wa Shuwasa Mhandisi Yusuph Katopola akizungumza. Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog Wananchi wa Manispaa ya Shinyanga wamependekeza kuanzishwa kwa mita za malipo ya kabla (prepaid water meters) ili kudhibiti malalamiko ya bili kubwa za maji, wakati wakisisitiza umuhimu wa kuimarishwa kwa huduma bora ya majisafi na usafi wa mazingira. Mapendekezo hayo yametolewa leo Machi 26, 2026, katika mkutano wa wadau wa maji ulioandaliwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga kwa lengo la kujadili rasimu ya mkataba mpya wa huduma kwa wateja. Mmoja wa wananchi hao, Ashirafu Said amesema licha ya maboresho yanayoendelea kufanywa na SHUWASA, bado kuna changamoto ya malalamiko ya bili zisizoendana na matumizi halisi ya maji. “Tunapongeza juhudi za SHUWASA, lakini tunaomba kuanzishwa kwa mita za malipo ya kabla ili kuongeza uwazi. Kama ilivyo kwenye umeme wa LUKU, tokeni ikiisha huduma inakatika, hivyo kuepusha bili kubwa zisizoeleweka,” amesema Ashirafu. Mgeni rasmi katika mkutano…