Viongozi wa Dini Watoboa Siri: Ndoa za Utotoni Zazidi Kushamiri Vijijini Licha ya Sheria
Viongozi wa Dini Watoboa Siri: Ndoa za Utotoni Zazidi Kushamiri Vijijini Licha ya Sheria
Dar es Salaam, Machi 28, 2026 — Viongozi wa dini nchini wameeleza wasiwasi wao kuhusu kuendelea kwa ndoa za utotoni, wakibainisha kuwa changamoto ya uelewa mdogo wa sheria kuhusu umri sahihi wa kuolewa bado ni kubwa, hasa katika maeneo ya vijijini. Akizungumza katika kikao cha kitaifa cha viongozi wa dini kuhusu mabadiliko ya kisheria ya ndoa kilichofanyika Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya BAKWATA, Sheikh Khamisi Mtaka, alisema pamoja na jitihada mbalimbali zinazofanyika kukomesha ndoa za utotoni, bado kuna mkanganyiko mkubwa kati ya sheria za nchi, mafundisho ya dini na mitazamo ya kijamii. Alisema hali hiyo imekuwa kikwazo kikubwa katika utekelezaji wa juhudi za kupambana na tatizo hilo. Sheikh Mtaka alifafanua kuwa kwa sasa hakuna sheria mahsusi inayokataza moja kwa moja ndoa za utotoni, isipokuwa Sera ya Elimu ya mwaka 2014 inayozuia wanafunzi kuolewa au kupata ujauzito wakiwa shuleni. “Endapo kipengele hiki kitaingizwa pia katika mifumo ya kijamii na kidini bila kukinz…