Ujenzi miundombinu ya BRT Awamu ya Tatu Gongo la Mboto wafikia 99%
Ujenzi miundombinu ya BRT Awamu ya Tatu Gongo la Mboto wafikia 99%
Na. Mwandishi Wetu. Awamu ya Tatu ya Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka maarufu kama Mwendokasi katika Barabara ya Nyerere kuelekea Gongolamboto na maeneo yaJirani sasa umefikia asilimia 99 kwa ujenzi wa Vituo vya Mabasi Pamoja na Barabara za zege. Akizungumza kuhusu maendeleo ya awamu hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Usafirishaji wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Bi. Delphina Pweleza amesema kuwa ujenzi wa awamu hiyo ya tatu ya BRT uligawanyika katika Lot 2 yaani ujenzi wa miundombinu ya Barabara na Vituo vyake ambao mpaka sasa umefikia asilimia 99% huku Lot ya 2 inayohusisha ujenzi wa Karakana, Kituo Kikuu cha Airport na kituo mlishi cha Banana ikiwa kwenye hatua za awali. “Kwa sasa ujenzi wa miundombinu ya barabara na vituo umekamilika kwa asilimia tisini na tisa (99%) na matarajio ya kukabidhiwa ikiwa ni mwishoni mwa mwezi April 2026” Alisema Bi. Pweleza. Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi wa Gongolamboto Jijini Dar es Salaam wamesema mradi huo utakapoanza kufnya kazi utakuwa…