TTCL NA T-PESA: UBABAISHAJI UNAOGHARIMU NA KUKWASHAMISHA UCHUMI WA KIDIJITALI
TTCL NA T-PESA: UBABAISHAJI UNAOGHARIMU NA KUKWASHAMISHA UCHUMI WA KIDIJITALI
Na Beda Msimbe Katika kuelekea kilele cha uchumi wa kidijitali, ni dhahiri kuwa kasi ya teknolojia lazima iende sambamba na kasi ya uwajibikaji. Hata hivyo, uzoefu wangu wa siku nne zilizopita na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kupitia huduma zao za T-Pesa na Faiba Mlangoni, umechora picha tofauti; picha ya ubabaishaji wa wazi unaogharimu muda, fedha, na ufanisi wa kazi wa mteja. Safari hii ya kutaabika ilianza Jumatano iliyopita baada ya kufanya malipo ya shilingi 55,000 kwa ajili ya huduma ya intaneti ya Faiba nyumbani kwangu, Goba. Licha ya fedha kukatwa katika akaunti yangu ya T-Pesa, hakuna muamala wowote uliofika upande wa huduma ya Faiba, na akaunti yangu ikabaki gizani. Nililazimika kusafiri kutoka Goba hadi Posta kutafuta ufumbuzi, ambapo maofisa walithibitisha kuonekana kwa fedha hizo na namba ya malipo (control number), lakini walishindwa kukamilisha muamala huo kwa saa mbili, huku wakiniahidi kuwa tatizo lingeshughulikiwa. Ahadi hiyo imekuwa wimbo wa kila siku usio na …