TRC YAWASHIKA MKONO WAATHIRIKA WA MAFURIKO IFAKARA -MOROGORO, MBUNGE ATOA WITO Na Fredy Mwanjala, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano, Shirika la Reli Tanzania (TRC). Wananchi wa kaya 150 za kata za Kibaoni, Michenga, Lumemo na Lipangalala katika Halmashauri ya mji wa Ifakara, Jimbo la Kilombero, Mkoani Morogoro, wamelishukuru Shirika la Reli Tanzania (TRC) kwa kuwapatia msaada wa tani kumi za unga, unaolenga angalau kupunguza adha, kufuatia mafuriko yaliyosababishwa na mvua iliyonyesha Machi 24 na 25, 2026. Msaada huo umepokelewa na Mbunge wa jimbo la Kilombero. Mheshimiwa Abubakari Asenga, mbele ya wananchi wa kata hizo katika hafla fupi iliyofanyika kijiji cha kibaoni, kata ya kibaoni, Halmashauri ya mji wa Ifakara, Mkoani Morogoro. Akizungumzia msaada huo, Mheshimiwa Asenga, amesema analishuru Shirika la Reli Tanzania, kuwasaidia wananchi wa Ifakara walioathirika na mafuriko hayo a kutoa wito kwa taasisi za umma na binafsi, mashirika kuiga mfano wa TRC. “Shirika letu la Reli limeonesha mfano mzuri sana, hiki walichokitoa ni kikubwa sana na wananchi wa Ifa…