TMA JNIA YATOA ELIMU KWA JAMII KUADHIMISHA SIKU YA HALI YA HEWA DUNIANI 2026
TMA JNIA YATOA ELIMU KWA JAMII KUADHIMISHA SIKU YA HALI YA HEWA DUNIANI 2026
Na Karama Kenyunko Michuzi Tv MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Kituo cha Hali ya Hewa cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), imeadhimisha Siku ya Hali ya Hewa Duniani kwa kutoa elimu kwa wadau pamoja na kuweka mipango ya kuendelea kutoa huduma bora, kuongeza tija na ufanisi, na kuhakikisha usalama wa usafiri wa anga kwa kutoa taarifa sahihi. Akizungumza leo, Machi 23, 2026, jijini Dar es Salaam wakati wa kutoa elimu kwa wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi waliotembelea Kituo cha Hali ya Hewa cha JNIA, Meneja wa TMA wa Huduma za Hali ya Hewa katika Usafiri wa Anga na Msimamizi wa Kituo cha Hali ya Hewa JNIA, John Mayunga, amesema kuwa ni muhimu kuelimisha jamii ili iweze kuchukua tahadhari na kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa. Mayunga ameongeza kuwa kuna mchango mkubwa wa utoaji wa tahadhari mapema kabla jamii haijakumbwa na athari za mabadiliko ya hali ya hewa, kwani majanga mengi duniani yamehusishwa na hali mbaya ya hewa. “Serikali imeendelea kufa…