TANZANIA YASISITIZA DHAMIRA YAKE KUENDELEZA DIPLOMASIA YA MAJI

TANZANIA YASISITIZA DHAMIRA YAKE KUENDELEZA DIPLOMASIA YA MAJI
Tanzania imesisitiza dhamira yake kuendeleza ushirikiano wa kikanda katika usimamizi wa rasilimali za maji katika Mkutano wa Maji wa Sululta na Diplomasia ya Maji (Sululta Water and Hydro Diplomacy Conference) uliofanyika katika Mji wa Bishoftu, nchini Ethiopia. Mkurugenzi wa Ubora wa Maji, Bw. Heri Chisute kwa niaba ya Waziri wa Maji, amesema mkutano huo wenye kaulimbiu “Diplomasia ya Maji na Ushirikiano wa Kikanda kwa Maendeleo Endelevu ya Maji na Nishati pamoja na Usimamizi Wake” unakumbusha maji ni zaidi ya rasilimali. ni uhai, daraja linalounganisha mataifa na msingi wa amani na ustawi.  “Kwa Tanzania ushirikiano wa kikanda wa majishirikishi ni ushuhuda unaoishi; kutoka Bonde la Mto Nile hadi Kamisheni ya Bonde la Mto Zambezi, Kamisheni ya Bonde la Mto Songwe hadi Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria, tumejifunza kwamba mataifa yanaposhirikiana kwenye eneo la majishirikishi, maji huwa chanzo cha umoja badala ya mgogoro”, Chisute amesema. Ameongeza Tanzania imejikita katika misingi mi…