TANZANIA YAONGEZA KASI KUTOKOMEZA KIFUA KIKUU; WITO WA USHIRIKIANO WATOLEWA

TANZANIA YAONGEZA KASI KUTOKOMEZA KIFUA KIKUU; WITO WA USHIRIKIANO WATOLEWA
Na John Mapepele Waziri wa Afya, Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa amesema Tanzania leo, Machi 24, 2026 imeungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha Siku ya Kifua Kikuu Duniani, siku maalum inayolenga kuongeza jitihada za kupambana na ugonjwa huu hatari unaoendelea kuathiri mamilioni ya watu duniani. Amewataka watanzania kuendelea kushirikiana na Serikali ili kutokomeza ugonjwa huo hapa nchini. "Ili kuhakikisha tunafanikiwa kutokomeza ugonjwa huu, jitihada za pamoja za wadau wote katika kuwajibika zinahitajika." Amesisitiza Mhe. Mchengerwa Aidha, katika tamko rasmi lililotolewa na Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Grace Magembe, Serikali imesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa pamoja katika kufanikisha azma ya kutokomeza kifua kikuu ifikapo mwaka 2030. Kauli mbiu ya mwaka huu, “Kwa Jitihada za Pamoja za Viongozi, Wadau na Wananchi, inawezekana Kutokomeza Kifua Kikuu nchini,” imebeba ujumbe mzito wa uwajibikaji kwa kila mmoja. Kauli hii inalenga kuwakumbusha viongozi, wadau wa maendele…